LYRICS: NICK WA PILI FT. CHINBEES ROLE MODEL



[Intro – ChinBees]
Mnaowaita role models ni hatari, hatari take care
Mnaowaita role models ni hatari, hatari take care
Mnaowaiga wote mtapotea, mtapotea
Mnaowaiga wote mtapotea
Mi sio role model, mtapotea

[Verse 1 – Nikki Wa Pili]
I say kama mdada kaa mbali no gway
Ukishoboka star nakufanya chai
Hakuna video bila demu kuwa uchi
Hakuna sanaa tena ya kukomboa nchi
Kuvuta bangi na unga umarekani nimeiga
Role model kitaani nna vijana wananiiga
Wanakwisha kwisha, wanatuiga kisa
Hawatujui kabisa kitabia, argh!
Skendo skendo sio kiki kiki
Hizo wengi wetu ndo tabia, argh!
Nana nasimbi Zanzibar ujamaa wa lakuda
Hizo haziuzi huku soko chura!
Nani role model? Wanasema yule sista
Mwingi wa makalio kwenye page yake Insta
Siishi uhalisia, uhalisia utani-cost
Bila nguo mpya siezi picha nika-post!

[Hook – ChinBees]
Mnaowaita role models ni hatari, hatari take care
Mnaowaita role models ni hatari, hatari take care
Mnaowaiga wote mtapotea
Mi sio role model, mtapotea
Mnaowaiga wote mtapotea
Mi sio role model, mtapotea

[Verse 2 – Nikki Wa Pili]
Waanzilishi magwiji, waasisi wa skendo
Za jiji ndo sisi magwiji, argh!
Ni role model labda kama umelewa, argh!
Role model jijini analelewa, elewa
Tumia kipaji sio mapaja, elewa
Sanaa ni maadili yenye haja, elewa
Sura yangu sio innocent, elewa
Sura yangu labda ni kisenti, elewa
Cent money, mapene church, elewa
Marry go round mapene siachi, elewa
We mwanafunzi wa sekondari, elewa
Ukiniiga ni posa bila mahari, elewa
Dhambi iki-hit kama Yesu, elewa
Haipaswi kuabudiwa sema yes

[Hook – ChinBees]
Ni hatari, hatari take care
Mnaowaita role models ni hatari, hatari take care
Mnaowaiga wote mtapotea
Mi sio role model, mtapotea
Mnaowaiga wote mtapotea
Mi sio role model, mtapotea

[Outro – Nikki Wa Pili]
Yeah!
Maisha yangu fake siwezi nikawa role model
Usibugie jiwe haliwezi likawa embe dodo
Hata nikiwa kwenye media naongea kauli ya kibiashara kulinda brand
Siongei ukweli, ha-ha
It’s the rap, man
Dave Makoo, ChinBees
Along side my boy, Easy William, eh
Tranquillity, cheese and brain
Afrocentric, you heard?
Ha-ha, you ain’t a role model, nigga
Share on Google Plus

0 comments: