Showing posts with label news. Show all posts
Ifahamu Album mpya ya Dj khaled 'Major Key'
Ile album iliyokuwa ikisubiliwa sana tayari imetoka
ikiwa na jumla ya nyimbo 14 akiwashirikisha wakali kama vile Jay Z, Lil Wayne, Drake, Nas, Jeezy, Travis Scott, Kendrick Lamar, Nicki Minaj, Future, Gucci Mane, J. Cole, Big Sean, Chris Brown, Wiz Khalifa, Wale, Rick Ross, Bryson Tiller, August Alsina, na wengine wengi album hii kaipa jina la major key,tayari inapatikana iTunes unaweza kusikiliza track zote 14 list yake ipo hapa chini
1. I Got the Keys (feat. JAY Z & Future)
2. For Free (feat. Drake)
3. Nas Album Done (feat. Nas)
4. Holy Key (feat. Big Sean, Kendrick Lamar & Betty Wright)
5. Jermaine’s Interlude (feat. J. Cole)
6. Ima Be Alright (feat. Bryson Tiller & Future)
7. Do You Mind (feat. Nicki Minaj, Chris Brown, August Alsina, Jeremih, Future & Rick Ross)
8. Pick These Hoes Apart (feat. Kodak Black, Jeezy & French Montana)
9. F**k Up the Club (feat. Future, Rick Ross, YG & Yo Gotti)
10. Work for It (feat. Big Sean, Gucci Mane & 2 Chainz)
11. Don’t Ever Play Yourself (feat. Jadakiss, Fabolous, Fat Joe, Busta Rhymes & Kent Jones)
12. Tourist (feat. Travis Scott & Lil Wayne)
13. Forgive Me Father (feat. Meghan Trainor, Wiz Khalifa & Wale)
14. Progress (Movado)
WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2016
Hatimaye serikali imetangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi ambapo jumla ya wanafunzi 64,961 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano kwa mwaka 2016 ikiwa ni ongezeko la asilimia 18.1 la ufaulu ikilinganishwa na mwaka jana idadi ya mwaka jana ambayo ni 55,003.
Akitoa taarifa kwa umma kuhusu matokeo hayo waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George Simbachawene amesema jumla ya wanafunzi 64961 wasichana wakiwa ni 28991 na wavulana 36050 ambao ni asilimia 71.98 ya wanafunzi 90284 waliostahili kuingia kidato cha tano mwaka 2016 wamechaguliwa kujiunga na masomo hayo kwa mwaka 2016 .
Kwa upande wa waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya ufundi waziri Simbachawene amesema jumla ya wanafunzi 759 wasichana 220 na wavulana 539 wamechaguliwa kujiunga na mafunzo hayo ambapo kutokana na ufaulu huo idadi ya wanafunzi wa kike imeongezeka kutoka 147 kwa mwaka 2015 hadi kufikia 220 mwaka huu ikiwa ni sawa na asilimia 49.66 .
Katika taarifa hiyo imebainisha pia muda wa wanafunzi kuripoti mashuleni kwa ajili ya kuanza masomo ni tarehe 25 july 2016 na endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti nafasi yake itachukuliwa na kupewa mwanafunzi aliyekosa.
Subscribe to:
Posts (Atom)



KAA KARIBU NA MIMI
Kazi yangu ni kuhakikisha hupitwi, kaa karibu na mimi kwa kubofya hapo chini ☟