ORWACHI (LOVE.POWER.FAMILY)

MWANDISHI:......................ELYAM.
E.CHEMPS
STORY: ............................ORWACHI
(Love, Power& Family)
INAPATIKANA PIA PAGE YA #STORY
ZA ELLY
SIMU:0673393509
SEHEMU....................(01)
HII NI SIMULIZI ILIYONIFANYA NIWE
MTU WA KUJISIKIA FARAJA KILA
MARA KUTOKANA NA UJUZI
NILIOTUMIA HUMU KUWA WA KIPEKEE
MAONI YAKO NA LIKE PIA NDO
ZINANIPA NGUVU KUFANYA HIVI KWA
HIYO UKIMALIZA LIKE NA UKOMENT
PIA BASI SHUKA NAYO...
Ilikua ni uzuni na pia fedhea kwa
mfalme aitwaye Orachi wa kijiji cha
Orwachi aliyeheshimika na kuogopeka
sana katika nchi hiyo kukosa mtoto wa
kiume wa kurithi nafasi yake japo tu
ikitokea akiaga dunia,basi aliamua
kumuita mganga aliyeitwa Kudusi
aliyeingia pale kwa mfalme na kumpa
heshima zake zote kisha akamsikiliza.
mfalme alianza"kudusi,nadhani unajua
fika heshima na sifa yangu
niliyojijengea hapa kijijini na nchini kote
na sasa inaonekana kushuka ghafla
kutokana na kitu ambacho zamani
nilikua naona kidogo lakini sasa
nimekoma kabisa"
"nadhani mfalme hauna haja ya
kuendelea mimi nimeshaanza
kukuelewa najua inaongelea swala zima
la mtoto mtukufu"
mfalme akashtuka na kuzidi
kumkodolea macho mganga huyp
kudusi naye mganga hakujali
akaendekea
"mtukufu najua fika kuwa hao wanao
ulionao wawili sio wa kiume ni wa kike
na hujali kabisa kuwa hawawezi
kuiongoza vyema Orwachi"
"lakini pia ntakua nimeenda kinyume na
miiko na sheria za kijiji hiki"alisema yule
mfalme
"ndio ni kweli lakini mfalme kwanini
usijaribu kuoa mwanamke wa pili
basi"mfalme akafyonza kisha
akamwangalia mganga na
kusema"katika washauri wangu wote
nilikua nakutegemea sana ujue kumbe
na wewe ni mbumbumbu tu
ninavyompenda mke wangu malkia
Evoke mama wa watoto wangu hata
siku moja siwezi kufanya kitu kama
hicho"kipindi anayaongea hayo kumbe
mke wake alikua anasikia kipindi chote
basi Nate hakusita kusema yake
akajitokeza na kumkatisha mfalme
"mme wangu kwanini usimsikilize
mganga tu"
"wewe hivi unaelewa unachoongea
ila"alijibu mfalme na kuendelea
"mke wangu hiyo itakua fedhea kwako
kwangu na watoto pia hawata nielewa
daima mke wangu "Mme wangu najua
wewe ndo mfalme unahitaji kupata
mrithi ili kijiji hiki kibaki na muongozo" basi mfalme alikua kama amezibwa
mdomo na mke wake na kukaa kimya
kisha akasema
"naomba kudusi niache nkijifikiria
ntakuita ili tufanye utaratibu"
mganga akaamka na kutupa neno la
mwisho
"ila mtukufu jitahidi sana kutoa uamuzi
sahihi juu ya hili"naye akamjibu
"wala usijali wewe kwa sasa naomba
uniache kwanza"mke wake
alimwangalia mme wake kwa uzuni
huku akijifikiria jinsi atakavyo vumilia
kuishi na mwanamke mwenzake pale
akijiuliza he upendo wa Mme wake
utabaki vilevile au utapungua,lakini kwa
upande wa mfalme yeye alikua hata
mawazo ya mke wa pili hana kabisa
alijisemea lazima iwrpo njia nyingine tu.
******************************
kesho yake mfalme alionekana
mnyonge na mwenye uchovu sana
kutokana na maneno Yale hasa
yaliyosemwa na mkewe,kwa kuwa
ndiye alikua anamwamini sana na
huyohuyo ndiye anayemuimiza afanye
hivyo pia anajua mke wake Evoke alikua
hahafikiani na hilo ila kamshauri tu ili
kukubaliana na hali kwamba yeye
amechoka na umri ulikua umeenda
sasa kiasi cha mke wake kutokua na
uwezo wa kutunga mimba baada ya
kushambuliwa na ugonjwa wa ajabu
uliofanya sejemu sake za uzazi
kupooza na hata yote waliambiwa na
mganga huyo huyo.Kipindi mfalme
akijifikiria ghafla alihisi kama kifua
kinabana akaanza kukohoa na
kuoumulia kwa chini sana hiki sauti
yake ikififia kwa mbali akarusha mikono
huku akijaribu kujiinua ila wapi kisha
akaanza kuona kama Giza hivi kama
vile malaika mtoa roho anamwita...
JE, MFALME ALICHUKUA UAMUZI GANI
BAADA YA HAPO FUATILIA TOLEO
LIJALO PIA USISAHAU KU LIKE NA
KUKOMENT KWA ULICHOSOMA
MAANA NDO NGUVU YANGU NI
"ORWACHI IPATE PIA KWENYE *STORY
ZA ELLY*PAGE

Share on Google Plus

0 comments: