Hatimaye serikali imetangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi ambapo jumla ya wanafunzi 64,961 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano kwa mwaka 2016 ikiwa ni ongezeko la asilimia 18.1 la ufaulu ikilinganishwa na mwaka jana idadi ya mwaka jana ambayo ni 55,003.
Akitoa taarifa kwa umma kuhusu matokeo hayo waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George Simbachawene amesema jumla ya wanafunzi 64961 wasichana wakiwa ni 28991 na wavulana 36050 ambao ni asilimia 71.98 ya wanafunzi 90284 waliostahili kuingia kidato cha tano mwaka 2016 wamechaguliwa kujiunga na masomo hayo kwa mwaka 2016 .
Kwa upande wa waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya ufundi waziri Simbachawene amesema jumla ya wanafunzi 759 wasichana 220 na wavulana 539 wamechaguliwa kujiunga na mafunzo hayo ambapo kutokana na ufaulu huo idadi ya wanafunzi wa kike imeongezeka kutoka 147 kwa mwaka 2015 hadi kufikia 220 mwaka huu ikiwa ni sawa na asilimia 49.66 .
Katika taarifa hiyo imebainisha pia muda wa wanafunzi kuripoti mashuleni kwa ajili ya kuanza masomo ni tarehe 25 july 2016 na endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti nafasi yake itachukuliwa na kupewa mwanafunzi aliyekosa.
0 comments: